Wakati Tanzania, ikianisha mikoa mitano iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola, kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo katika mji wa Mubende nchini Uganda, mamlaka ya afya mjini Busia mpakani mwa Kenya imeongeza jitihada za kuzuia virusi hivyo visisambae kwa wakazi wa eneo hilo au zaidi.
Kaimu Afisa Mkuu wa Usafi wa Mazingira kaunti ya Busia, Dkt. Melsa Lutomia amesema uchunguzi na upimaji wa afya umekuwa ukifanyika kwa kila anayepitia mpakani kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi, Sudan Kusini, na Uganda ili aweze kuwa na sifa ya kuingia Kenya kwa kuwahusisha wataalamu wa afya.
Amesema, “Kwa hivyo, kinachofanyika ni kupima halijoto baada ya hapo wateja kujaza fomu ya uchunguzi na kimsingi wanajaza taarifa zao binafsi kama vile majina yao na mawasiliano na walikoanzia safari ili tuweze kubaini kama wanatoka maeneo yoyote karibu na tarafa ya Mubende nchini Uganda.”
Wakati Tanzania, ikianisha mikoa mitano iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola, kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo katika mji wa Mubende nchini Uganda, mamlaka ya afya mjini Busia mpakani mwa Kenya imeongeza jitihada za kuzuia virusi hivyo visisambae kwa wakazi wa eneo hilo au zaidi.
Kaimu Afisa Mkuu wa Usafi wa Mazingira kaunti ya Busia, Dkt. Melsa Lutomia amesema uchunguzi na upimaji wa afya umekuwa ukifanyika kwa kila anayepitia mpakani kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi, Sudan Kusini, na Uganda ili aweze kuwa na sifa ya kuingia Kenya kwa kuwahusisha wataalamu wa afya.
Hata hivyo, anasema licha ya kuwachunguza zaidi ya watu 5,000 tangu kisa cha kwanza cha Ebola kuripotiwa nchini Uganda takriban wiki mbili zilizopita, hakuna aliyekutwa na dalili za maradhi hayo ingawa wengi wa wananchi wanaosafiri wamekuwa na hofu akiwemo
Dereva wa lori, George Mwangi aliyesafiri kutoka Kenya kwenda Uganda.
Mwangi anasema, “Wakazi wa hapa Busia wana wasiwasi maana watu wengi huvuka mpaka huu kutoka Kongo, Rwanda, Burundi, Tanzania sasa nataka kuiomba Serikali ichukue hatua kali la sivyo tutaathirika pakubwa na tukipata ugonjwa huo tunaweza kuusambaza katika miji mingine na watu wengi watakufa.”