Mwakilishi wa kanda ya Afrika, wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), Abebe Haile-Gabriel amewaambia wajumbe katika mkutano nchini Nigeria kuwa suluhisho endelevu la uhaba wa chakula Duniani ni amani.

Haile-Gabriel, ameyasema hayo wakati akiwa katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja kujadili usalama wa chakula na njia ya kufikia lengo la sifuri la njaa na wadau wa ndani kujadili uwekaji wa juhudi za kuhamisha miongo kadhaa iliyopita ya ukame na migogoro, ikiwa ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka 10 ambapo baadhi ya mataifa yanatishiwa na baa la njaa.

Mazungumzo hayo, yanakuja ikiwa ni siku chache baada ya Umoja wa Mataifa kuonya kuwa mamia ya maelfu ya watu nchini Somalia wanakabiliwa na njaa ambapo amesema, “Hali nchini Somalia ni mbaya. Kumekuwa na ukame kwa zaidi ya miaka minne mfululizo na hii ina madhara makubwa kwa maisha ya watu wa huko.”

Ukame mkali kuwahi kutokea, katika Pembe ya Afrika umeharibu mazao na kuua mifugo ambayo maisha ya watu katika eneo hilo yanategemea ambapo Haile-Gabriel anasisitiza ukweli kwamba, ili kufikia usalama wa chakula kunahitaji zaidi ya msaada kwa wakulima huku FAO ikishirikiana na baadhi ya mashirika ya wafadhili kutafuta amani.

Akizungumza hivi majuzi kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alitoa wito kwa washirika wa nchi hiyo kufanya kila linalowezekana ili kuepusha baa la njaa, ambalo pia linatishia eneo kubwa la Pembe ya Afrika jambo litakalookoa maisha ya watu na kuleta hali ya utulivu.

Maradhi afya ya akili sehemu za kazi ni tatizo
DRC yasema imehitimisha rasmi Ebola