Madereva wa daladala zinazofanya kazi yake katikati ya jiji la Tanga wameendelea na mgomo wao ulioanza jana asbuhi mkoani humo.
Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, ambapo amesema kuwa madereva hao wamegoma kufanya kazi kwa kile kinachodaiwa kupinga uonevu unaofanywa na Askari wa kikosi cha usalama barabarani ambao wamekuwa wakiwatoza faini na kuwakamata bila makosa.
“Ni kweli madereva wamegoma tangu jana lakini wengine kwenye baadhi ya maeneo wameanza kazi leo na wengine bado wamegoma na tunatarajia kukutana nao asubuhi hii kwaajili ya kuzungumza namna ya kutatua mgomo huo,” amesema RPC Wakulyamba.
Hata hivyo, Mapema wiki iliyopita RPC Wakulyamba alithibitisha kukamatwa kwa madereva kumi wa mabasi na daladala kwa tuhuma za kuendesha vyombo vyao bila kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani
-
RC Makonda apewa msaada na benki ya PBZ
-
NEC yaruhusu leseni ya udereva kupigia kura
-
Whatsapp yamponza Mbunge