Chama cha madereva wa Bajaji Manispaa ya Iringa wamehimizana kuacha kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa abiria wao na kwamba hawatamvumilia mtu yeyote ambaye atakiuka mpango huo.

Mwenyekiti wa chama hicho, Melabu Kihwele akiongea wakati wa ziara ya kuzungukia maegesho ya Bajaji kwa nyakati tofauti alisema uongozi wao  umedhamiria kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Baadhi ya Madereva wa Bajaji Mkoani Iringa waliojitokeza kupinga ukatili wa Kijinsia.

Amesema, wao Kama wanaumoja wa Bajaji Mkoani Iringa wanayo dhamira ya dhati ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupinga vitendo vya ukatili kwa Watoto na wanawake, ambavyo kwa siku za hivi karibu vimezidi kuongezeka.

Alisema kuwa Dereva Bajaji yoyote atakaye baka au kulawiti hawatamfumbia macho kwa kuharibu taswira yao kama ambavyo imetokea kwa siku za karibuni kwa Dereva Bajaji wa Manispaa ya Iringa amefungwa miaka 30 jera kwa kosa la ukatili wa kijinsia.

Huduma ya kujipima VVU yasogezwa mahala pa kazi
ZRA yajipanga kuongeza wigo wa mapato