Scolastica Msewa – Kigamboni.
Madrasat Hidaya Islamic Centre ya Kigamboni jijini Dar es salaam inatarajia kuongoza Waislamu na dini zingine nchini, kufanya ibada maalumu ya kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Dkt. Hussein Ally Mwinyi na Taifa, ili Mwenyezi Mungu aendelee kutupa heri, Upendo na mshikamano.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Dua maalumu ya kuombea taifa na Viongozi wa nchi, Omary Kombe wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Madrasat Hidaya Islamic Centre huko Kigamboni jijini Dar es salaam.
Amesema Dua hiyo maalumu itafanyika Oktoba 7, 2023 katika Viwanja vya Mnadani vilivyopo Darajani Kigamboni jijini Dar es Salaam, kwa kushirikisha vituo vya kulelea watoto yatima, viongozi wa Dini, Serikali, Vyama vya Siasa na Jamii kwa ujumla.
“Hivyo tunachukua fulsa hii kuwaalika watu wote kushiriki kwa pamoja ili kuliombea taifa letu kwani tunatambua kazi kubwa na majukumu waliyo nayo Viongozi wetu katika kuliomgoza taifa letu la Tanzania, sisi kama sehemu ya jamii tunaowajibu na Haki ya kuliombea taifa na Viongozi wake,” alisema.
Aidha, akizungumzia masuala ya ukatili wa kijinsia na ukosefu wa maadili katika jamii Omary amesema, “Watanzania tudumishe Mila na destuli zetu ikiwa ni kuthibiti na kukabiliana na janga kubwa la ukatili wa kijinsia na ukosefu wa maadili katika taifa letu.
Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya Hidaya Islamic Centre ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Twahili Shaibu amesema Dua hiyo itahusisha Watanzania wote bila kujali tofauti za kidi kwani lengo ni kuombea Viongozi na taifa letu kwa ujumla na kwamba Watanzania waliombee Taifa hasa kutokana na taarifa za kuwepo kwa mvua za elnino, ili zisilete madhara nchini.