Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo amewaomba waumini wa kanisa la Evangelist Asemblies of God EAGT la Mafinga kuendelea kuliombea Taifa .

Chongolo amewaomba waumini hao wa EAGT Mafinga kumuombea Rais Dokta Samia Suluhu Hassan ili aendelee kulitumikia Taifa hasa katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Ametoa ombi hilo leo Mei 28,2023 aliposhiriki ibada fupi katika kanisa la EAGTĀ  Mafinga akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya siku saba Mkoani Iringa ya kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020- 2025.

Amesema watanzania wanajukumu la kuliombea Taifa la Tanzania ili amani na utulivu viendelee kuwepo.

Katika hatua nyingine Chongolo amekabidhi kiasi cha Shilingi milioni mbili, fedha ambayo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt Samia Suluhu Hassan ambae ni Rais wa Tanzania kwa ajili ya kuendelea kumalizia ujenzi wa kanisa hilo la EAGT Mufindi ambapo ujenzi upo katika hatua za mwishoni.

Aliyempiga mke wake na kumngā€™oa jino akamatwa
Kocha USM Alger amuhofia Foston Mayele