Bosi wa Tottenham Hotspur, Daniel Levy amefunguka kuhusu miaka yake 15 ya kuiongoza timu hiyo bila ya taji na hatima ya Mshambuliaji Harry Kane na jinsi moyo unavyouma kwa mafanikio ya Arsenal.

Mwenyekiti huyo wa Spurs, Levy yupo kwenye klabu hiyo ya London Kaskazini tangu mwaka 2001 na kushuhudia mabadiliko kibao.

Amefuta makocha wa kudumu 11, amejenga uwanja mpya wa kisasa kabisa huku akiongoza timu, hiyo kwenye kubeba Kombe la Ligi 2008, ikimaliza ya pili kwenye Ligi Kuu England 2017 na kufika fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya 2019.

Lakini, mashabiki wa Spurs wanalia na timu yao kukaa muda mrefu bila ya taji tangu walipobeba Kombe la Ligi. Na kinachowauma zaidi ni kuona mahasimu wao Arsenal wakiwa pazuri kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Lakini, Levy mwenye umri wa miaka 61, amewataka mashabiki hao kukumbuka tu ilipotoka klabu hiyo, aliposema:”Tulipokuja Tottenham kwa mara ya kwanza, tulihitaji kushinda ili tubaki kwenye ligi.

Kisha tukaanza kupata mafanikio kucheza kwenye Europa League na kisha Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lengo letu kubwa ni kushinda mataji. Hilo ndilo tunalojaribu kulifanya. Ni rahisi kusema kuliko kufanya.”

Zinchenko arudi kundini Arsenal
Meridianbet Kasino Yaja na  mchongo mpya