“MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI”
Na Haji Manara
Inawezekana utawala wao hauna mbwembwe kama za Haji Manara, na umekosa umaarufu kwa baadhi ya Mashabiki wa soka nchini, lakini nathubutu kuandika utawala huu wa sasa wa Shirikisho la Soka nchini TFF ndio utawala unaoonyesha mafanikio makubwa ya maendeleo ya uwanjani Kwenye mchezo huu kuliko utawala wowote huko nyuma.
Hebu tuanzie miaka ya sitini baada ya uhuru hadi sasa na tukiyatembelea maneno ya Chairman Mao ya “No research No Data No right to Speak” Nani anaweza kulinganisha mafanikio ya utawala huu wa sasa wa TFF na zilizopita?
Ngoja nikueleze machache kisha unijibu swali langu pendwa,
Kwa mara ya kwanza baada ya Uhuru,Tanzania imeandaa Mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF ( Afcon Under 17 ) Baada ya miaka thelathini na tisa Tanzania imeshiriki fainali za Mataifa ya Afrika, Baada ya miaka kumi Tanzania inarejea tena Kwenye Mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ( CHAN).
Hapa sote tunajua yaani kufuzu kwetu kwa AFCON na CHAN ni ndani ya mwaka mmoja huu wa 2019, haipo TFF yoyote huko nyuma na hata tukisema FAT iliyowahi kuiwezesha nchi hii kubwa kufuzu katika mwaka mmoja Mashindano hayo yote kwa wakati mmoja (FACT ISIYOGUSIKA)