Hospital Kuu ya Jeshi la Polisi iliyopo Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam, itanufanika na mafunzo ya siku mbili yanayotolewa na shirika la Quality Heathcare Solution and Consulting – QHSC, ili kuwajengea uwezo katika kutoa huduma za kiafya.

Akiongea mara baada ya mafunzo kwa Madaktari na wauguzi kutoka Hospital kuu ya Jeshi la Polisi, Dkt. Harrieth Kokushubila Gabone amesema mafunzo hayo yatawanufaisha Wananchi wenye magonjwa ya moyo, wanaofika kupata huduma Hospitalimi hapo.

Kwa upande wake Daktari mfawidhi wa hospital kuu ya Jeshi la Polisi Dkt. Nyanda Lushina amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwaleta wataalam hao, huku akisema mafunzo hayo yatawajengea uwezo mkubwa kiutendaji.

Naye Mrakibu mwandamizi wa Polisi, SSP Emmanuel Shija amelishukuru shirika hilo kutoka Marekani kwa kutoa elimu ambayo imekuja kwa wakati muafaka, kwani wamekuwa wakipokea wagonjwa wenye changamoto ya magonjwa ya moyo.

Awali, Konstable wa Polisi Dkt. Davis Mwita wa kitengo cha Dharura Hospital kuu ya Jeshi la Polisi alisema mafunzo hayo yamewaongezea ujuzi na maarifa watakaotumia pindi wanapotoa huduma kwa Askari na Wananchi wanaofika Hosptalini hapo.

Wanawake watakiwa kuwa imara kuwalinda Watoto
Arsenal yajitosa tena kwa Dusan Vlahovic