Serikali imetuma timu maalum kwenda Mkoani Kilimanjaro kuchunguza tuhuma juu ya wanafunzi kufundishwa vitendo kinyume cha maadili katika baadhi ya shule.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo jijini Dodoma na kuongeza kuwa timu hiyo inaongozwa na Kamishna wa Elimu nchini, Mwanasheria wa Wizara hiyo na Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora.
Amesema, “Tumeshtushwa sana na jambo hilo, tumelichukua suala hili kwa umuhimu mkubwa tumeongea na mkuu wa mkoa na kama kuna jinai yeyote basi hatua za kisheria zichukuliwa mara moja.”
Aaidha, Wairi Mkenda amesema Wizara itatoa namba maalum ili kuwezesha wananchi kutoa taarifa za vitendo viovu vinavyochafua taswira ya elimu, na kwamba timu hiyo tayari imeanza uchunguzi katika shule zilizotajwa na hatua za haraka zitachukuliwa kwa wahusika.