Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Ally Shaban Kamwe amesema hatazungumza lolote kuhusu Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’.

Young Africans iliingia kwenye mtafaruku na Kiungo huyo, baada ya kujaribu kuvunja mkataba mwishoni mwa mwaka 2022, lakini suala hilo lilimalizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, japo Fei Toto ameendelea kususia kujiunga na wenzake kambini.

Ally Kamwe amesema suala la Fei Toto hatalitoa maelezo yoyote na badala yake amewataka Waandishi wa Habari kumuuliza kuhusu Wachezaji wengine ambao wamejitolea kuipambania timu.

“Kuanzia leo msiniulize maswali kuhusu Feisali, mniulize kuhusu wachezaji wanaojitoa kuipambania timu yetu, wanaotoa Jasho kwa ajili ya Young Africans” amesema Ally Kamwe

Fei Toto kwa sasa yupo nyumbani kwao Kisiwani Ungunja ‘Zanzibar’ akifanya mazoezi yake binafsi, huku ikielezwa huenda Wanasheria wake wakalipeleka suala lake mbele ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ‘CAS’.

Wanafunzi wa kike waomba msaada waendelee na masomo
Mafunzo ya uovu: Serikali yatuma timu Kilimanjaro