Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodgar Tenga ameteuliwa kuongoza Kamati ya Taifa ya Maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2027’ pamoja na ya wachezaji wa ndani ‘CHAN 2024’.

Uteuzi huo umefanywa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Damas Ndumaro pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tabia Maulid Mwita.

Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ lilikubali ombi la nhi za Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa kwa pamoja fainali hizo za AFCON 2027.

Kamati hiyo itakuwa na makujumu ya kufanya maandalizi ili kufanikisha mashindano hayo makubwa Barani Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, viongozi wengine walioteuliwa na nafasi zao katika mabano ni, Ayoub Mohammed Mahmoud (Makamu Mwenyekiti), Neema Msitha (Katibu), Said Kassim Marine (Katibu Msaidizi).

Wajumbe wa kamati hiyo ni Wallace Karia, Suleiman Mahmoud Jabir, Nehemia Msechu, Wilfred Kidao, Ally Mayay, Ameir Mohamed Makame, Naima Said Shaame, Mohamed Abdulaziz, Madundo Mtambo, Jacquline Kawishe, Gilead Teri na Aboubakar Bakhresa.

Wengine ni Profesa Mohamed Janabi, Abubakar Liongo, Thomas Ndonde, Rona Lyimo, Ramadhan Dau, Hassan Mabena, Abdul Nsekela, Jumanne Muliro, Abdul Mhinte, Saleh Ally, Hamad Abdallah, Johnson Pallangyo na Kheri Salum Ally.

Tayari Serikali imeanza ujenzi wa kiwanja cha Samia Suluhu Hassan jijini Arusha pamoja na kuanza kuvifanyia ukarabati mkubwa viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya mashindano hayo ya AFCON 2027.

Mbali na kiwanja hicho cha Samia, viwanja vingine vinavyotarajiwa kutumika kwa mashinadano hayo ni Benjamin Mkapa cha Dar es Salaam pamoja na Amaan, Zanzibar.

Ibenge kuikacha Al Hilal, atajwa Simba SC
Kisa Maji: Picha jongefu kutumika ukaguzi wa Miradi