Kufuatia marufuku ya utawala wa Taliban nchini Afghanistan ya Wanawake kutoruhusiwa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu, Wanafunzi wa kigeni ambao walikuwa wakisomea udaktari nchini humo wameomba msaada ili waweze kuendelea kupata Elimu.

Hatua hiyo, ilisababisha Wanafunzi wa kike 105 wa vyuo vikuu vya Afghanistan toka jimbo la magharibi la Pakistan, Khyber-Pakhtunkhwa, kufanya maandamano katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad, wakiomba msaada kwa jumuiya ya kimataifa.

Wanafunzi wa Kike wakimsikiliza Mwalimu Darasani. Picha ya BBC.

Hata hivyo, waandamanaji hao wametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kusaidia suala hilo na kuiomba Serekali ya Pakistan kutoa ufadhili maalumu kwa wanafunzi walio katika vyuo vya umma vya udaktari.

Mpaka sasa hakuna Serikali yeyote ambayo imeutambua utawala huo wa Taliban, kutokana na wasiwasi, ukiukwaji wa haki za binadamu na namna wanawake wanavyo tendewa ukatili huo wa kukosa elimu na uhuru nchini Afghanistan.

Mwambusi afunguka kuondoka Ihefu FC
Ally Kamwe: Msiniulize ya Fei Toto