Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda akiwa na ujumbe wake uliowasili Wilayani Hanang’ wamepatwa na simanzi walipomuona Mama aliyejifungua baada ya kuokolewa kwenye tope lililosababishwa na mafuriko.
Chatanda alikumbwa na hali hiyo baada ya kufika katika Kituo cha Afya cha Gendabi na kusema, “nimeshindwa kujizuia mimi kama Mama nikajikuta nalia kwa uchungu kuona Mwanamama huyu ambaye alisombwa na tope na kuweza kuokolewa kwenye tope hilo na kufikishwa hospital masaa mawili baadaye kujifungua salama.”
Mama huyo alijifungua Mtoto wa kiume Desembq 3, 2023 na Kilio cha Chatanda kilikuja baada ya kusikiliza simulizi za Mama huyo jinsi ambavyo alihangaika kuokoa watoto wake wawili huku akiwa mjamzito wa miezi tisa.
Kufuatia tukio hilo, UWT imesema itafanya jitihada kuhakikisha wanamuongezea mahitaji ya kutosha
Mama huyo ambaye kwa sasa yeye na familia wanalala hospitali kutokana na kukosa Makazi.