Lydia Mollel- Morogoro.

Ofisi ya Waziri  Mkuu  Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imesema Tanzania ina uwezo wa kukuza uchumi wake kutokana na Rasilimali zilizopo ,Wadau wa  Maendeleo waliopo pamoja na utayari wa Watanzania, hasa kwa kuwachukulia hatua wale ambao watakwamisha juhudi za Serikali za kukuza Uchumi wake.
 
Hayo yamebainishwa Mkoani Morogoro na Naibu Waziri Ofisi  ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi wakati ufunguzi wa kikao kazi cha Mradi wa USAID Kijana Nahodha kwa ajili kupokea taarifa ya utafiti wa soko la ajira.
 
Aidha kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya vijana hapa Nchini ambao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira Naibu Waziri Katambi amesema Ofisiya  Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imefanikiwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana 134,093 ili waweze kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa Ajira.

Awali, akitoa taarifa ya taarifa ya utafiti wa soko la ajira kupitia Mradi wa USAID Kijana Nahodha Mkurugenzi Msaidizi wa Mradi wa USAID Kijana Nahodha   Nehemiah Kahakwa amesema kupitia huo  umewasaidia vijana na kuwaandaa  kuingia katika ajira binafsi au kuajiriwa.
 
Nao vijana wanaonufaika na Mradi wa Kijana Nahodha unaofadhiliwa  na USAID wamesema kuwa Mradi huo unawanufaisha na mambo mbalimbali ikiwemo kukutanishwa na wadau lakini pia kushiriki katika maonyesho ya vijana kwa lengo la kuonyesha ujuzi walio nao lakini pia kujifunza kutoka kwa wenzao .

Mafuriko Hanang' yamliza Mwenyekiti UWT
Wananchi tulinde miundombinu ya Umeme - Kapinga