Takriban watu 15 wamefariki magharibi mwa nchi ya Uganda, baada ya maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa na kufunika nyumba zao, huku waokoaji wakiendelea kuchimba matope kutafuta manusura.

Maporomoko hayo ya ardhi, yanadaiwa kuwa ni ya kawaida katika eneo hilo la Kasese, ambapo ajali hiyo iliwahi kutokea hapo awali katika maeneo hayo na yale ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mvua hizo, zinakuja kufuatia ukame wa muda mrefu wa hivi majuzi, mvua kubwa kunyesha katika maeneo ya Uganda tangu mwishoni mwa mwezi Julai, na kusababisha mafuriko, vifo, uharibifu wa miundombinu, mazao na nyumba.

Takriban watu 24, waliuawa katika Wilaya ya Mbale iliyopo eneo la mashariki mwa Uganda mwezi Julai kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa kwenye eneo hilo.

Awali, Shirika la hali ya hewa nchini humo, lilitoa onyo na kuwashauri wakazi wa maeneo ya milimani kuwa waangalifu au kutafuta maeneo salama, kutokana na mvua kubwa ambazo zinaweza kusababisha uharibifu kuanzia Agosti hadi Desemba.

Kocha Katwila asubiri hatma yake Ihefu FC
Ahmed Ally awajibu mashabiki wanaomkataa Matola