Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye amemfuta kazi Waziri Mkuu na msaidizi wake Mkuu katika msako wa ngazi ya juu baada ya kuonya kuhusu njama ya mapinduzi dhidi yake.

Waziri Mkuu huyo, Alain Guillaume Bunyoni na Mkuu wake wa Baraza la Mawaziri, Jenerali Gabriel Nizigama wamefutwa kazi ikiwa ni hatua ya uwepo wa taharuki katika nchi hiyo, yenye historia ya machafuko Afrika ya kati.

Katika kikao cha bunge kilichoitishwa kwa dharula, Wabunge waliidhinisha uteuzi wa Waziri wa usalama Gervais Ndirakobuca kuchukua nafasi ya Bunyoni kama waziri Mkuu, baada ya kupata kura 113 za ndiyo zilizopigwa.

Kuondoka kwa Bunyoni, kulikuja baada ya Ndayishimiye ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka miwili, wiki iliyopita kuonya kuhusu njama ya mapinduzi dhidi yake.

Ndashimiye alionya na kusema, “Unafikiri jenerali wa jeshi anaweza kutishiwa kwa kusema watafanya mapinduzi? Mtu huyo ni nani? Yeyote huyo anapaswa kuja na kwa jina la Mungu, nitamshinda.”

Mwaka 2015, aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Piere Nkurunziza, alianzisha msako mkali dhidi ya wapinzani wa kisiasa ambao ulisababisha vifo vya watu 1,200 ambapo pia mauaji ya kikabila na vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika 2006 kusababisha vifo vya watu 300,000.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 08, 2022
Kenya: Jaji Mkuu amtaja Mungu hukumu ya kupinga matokeo