Mtu mmoja amefariki, katika ajali iliyohusisha magari matatu likiwemo basi la abiria kampuni ya BM lenye namba za usajili T 959 DDE, lililokua linatokea Dar kuelekea Turiani, gari ndogo aina ya Nissan Mistubishi yenye namba za usajili T 847 CWN na gari lingine Lori ambalo namba zake hazijafamika mara moja.

Mwakilishi wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa Morogoro, Ahmed Remba amesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Makungaya Manispaa ya Morogoro, barabara kuu ya Morogoro – Dodoma ambapo baada ya ajali kutokea, dereva aliondoa gari eneo la tukio la magari hayo yalikuwa yakitokea Dar es Salaam, kuelekea Dodoma.

Amesema, chanzo Cha ajali hiyo ni dereva wa Lori kusimama galfa na ndipo dereva wa gari dogo akagonga kwa nyuma Lori hilo Kisha nae kugongwa kwa nyuma basi hilo la BM.

Amemtaja mtu aliyepoteza maisha kuwa ni dereva wa gari dogo aina ya Nissan Mistubishi ambaye amefahamika kwa jina moja la Alfonce, huku abiria wote waliokuwa ndani ya Basi la BM wakitoka salama.

Teknolojia ya Habari kuinufaisha nchi kiuchumi
Matrekta yatajwa chanzo cha ajali Barabarani