Meneja wa Ukaguzi wa bidhaa zinazotoka Nje ya Nchi wa TBS Mhandisi Said Issa Mkwawa amesema kuwa kuanzia Julai 20, 2022 magari yote yaliyotumika yanayotoka nchini Japan yatakuwa yanakaguliwa nchini huko na kila gari litakaguliwa kwa dola za kimarekani 150 kabla ya kuja Tanzania.

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ameeleza kuwa ukaguzi wa magari hayo utafanywa Nchini na Kampuni ya EAA Company Limited ya nchini Japan.

Amesema kuwa taratibu za kuipata kampuni hiyo zimetumika kwa mujibu wa sheria za nchi na vigezo vilivyokuwa vimeanishwa vimefuatwa na kampuni hiyo.

Mhandisi Mkwawa ameongeza kuwa utaratibu huo utasaidia kuepuka gharama za matengenezo kwa wanunuaji wa magari ambacho kilikuwa kilio cha wadau wetu wa waagizaji na wauzaji wa magari

Amesema Shirika linaendelea na taratibu za kupata mawakala kwa ajili ya ukaguzi wa magari yanayotoka Nchi za Uingereza, Dubai na Singapore na utaratibu huo utakapokamilika basi waingizaji na wafanyabiashara wa magari watapewa taarifa.

Aidha kwa magari yaliyoko njiani na meli yatakaguliwa yakifika nchini kwani zoezi hilo kwa tararibu za kampuni ya ukaguzi umeanza Julai 20 mwaka huu.

Serikali kusimamia miradi ya madini mkakati
Manara aibuka na kumshukuru MUNGU