Majumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Crescentius Magori anaamini Kikosi cha klabu hiyo kina nafasi kubwa ya kufikia lengo la kucheza Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2022/23.

Simba SC ipo katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya Makundi ya Michuano hiyo, kufuatia ushindi wa 3-1 dhidi ya Primero de Agosto ya Angola, huku timu hizo zikitarajia kucheza mchezo wa Mkondo wa Pili Jumapili (Oktoba 16), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Simba TV, Magori amesema Simba SC ina kikosi Bora na Imara msimu huu, na Uongozi unaaamini kama utapata nafasi ya kusajili baadhi ya wachezaji wenye kiwango cha juu wakati wa Dirisha Dogo kikosi chao kitavuka lengo na kutinga hatua ya Fainali.

“Tukifanikiwa kufika hatua ya Makundi kwa hii timu tuliyonayo na mwezi January ( Dirisha dogo la usajili ) tukaongezea vitu kidogo tu tutafikia lengo letu la kucheza Nusu Fainali ama Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika,”

“Tuna Wachezaji wenye uzoefu mkubwa sana katika Michuano hii ya Afrika, msimu huu tumedhihirisha kwa kushinda michezo miwili mfululizo ugenini, hata tukiingia hatua ya Makundi hili tutaliendeleza ili kuvuka idadi ya alama ambazo tuliwahi kuzipata huko nyuma tulipocheza hatua hii.” amesema Magori

Simba SC imewahi kufika Hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa BArani Afrika mara mbili msimu wa 2018/19 na 2020/21, huku wakifanya hivyo kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita 2021/22.

Geoffrey Lea: Al Hilal ina faida kubwa
Wauguzi mbaroni tukio mtoto mchanga kunyofolewa viungo