Rais John Magufuli ameanza kufanya mabadiliko kwenye Jeshi la Polisi nchini kwa lengo la kuliboresha zaidi.

Taarifa za kuaminika zimeeleza kuwa Rais Magufuli amemteua Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, kuwa Kamishna mpya wa jeshi la Zima Moto na Uokoaji.

Chagonja anao uzoefu wa kutosha katika oparesheni za Polisi kwa kuwa ameshika nafasi ya Ukamishna wa Operesheni na Mafunzo tangu kipindi cha IGP mstaafu Said Mwema.

“Kama unavyojua, rais Magufuli anaenda na falsafa yake ya ‘Hapa Kazi Tu’, inaonekana amedhamiria kuboresha maeneo yote, leo inaweza kuwa wizara hii, kesho wizara ile,” kilisema chanzo cha kuaminika.

Waliokwepa Kodi Wajisalimisha, Walipa Mabilioni, Majina Yao Yako Hapa
Kimbunga Cha Magufuli Chawapitia Vigogo watatu Mwanza