Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amewashauri Baraza Kuu la Makanisa ya Kipentekoste TAG kuelekeza nguvu katika ujenzi wa viwanda ni baada ya kanisa hilo kueleza limetenga eneo kwaajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu.
Ametoa kauli hiyo leo Agosti 14. 2020 katika ukumbi wa Chuo cha Kibiblia miyuji jijini Dodoma, katika mkutano mkuu wa kanisa hilo.
“Nataka nikuhakikishie Askofu Mkuu tuko pamoja katika hilo, na mimi nafikiri sio tu lakini mnaweza kutenga eneo kwaajili ya kujenga viwanda. Hata kama ungeanzisha kiwanda cha kuchimba chuma kule Manda ili sisi Tanzania tusiwe tunaagiza chuma kjutoka kule nje. Tuchimbe chuma ambayo ni First Class yenye madini mbalimbali na viwanda vile vikawa chini ya TAG”. Amesema Rais Magufuli
Rais Magufuli ametoa shukrani kwa dini na madhebu yote nchini kwa mchango wanao toa kwa nchi na kutambua mchango wa taasisi za kidini na kuhaidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na kulinda na kuheshimu haki ya uhuru wa kuabudu kwa kila rai.
Ameongeza kuwa serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri ili kuwezesha taasisi za kidini kuendelea kuchangia maendeleo ya nchi.
Uongozi wa TAG umeipongeza serikali kwa kuweka nidhamu katika utendaji wa kazi kwenye sekta mbalimbali za serikali.