Hatimaye leo inaandikwa historia mpya Tanzania ambapo Rais John Magufuli anatarajiwa kuzindua rasmi daraja la Kigamboni ambalo ni kivutio kikuu hivi sasa jijini Dar es Salaam.

Daraja la Kigamboni

Daraja hilo lililoanza kujengwa rasmi Februari 2012 linafunguliwa rasmi leo, likiwa na urefu wa Mita zaidi ya 600 likiungwa na barabara zenye urefu wa Kilometa 2.5 likiunganisha eneo la Kigamboni na katikati ya jiji la Dar es Salaam kupitia eneo la Kurasini.

Adha ya usafiri kwa wakazi wa Kigamboni kuingia katikati ya jiji itakuwa historia kwani daraja hilo linatoa nafasi kwa waenda kwa miguu kupita bila malipo yoyote huku magari yakitozwa kiasi cha fedha kinachosaidia uendeshaji wa daraja hilo.

Mtanzania awa muafrika pekee kubeba tuzo hii kubwa zaidi duniani
Video: Rais Magufuli amuapisha Balozi Chikawe