Mahakama nchini Kenya imepinga agizo la Serikali ya nchi hiyo la kupiga marufuku matumizi ya mifuko aina ya plastiki ambayo ilikuwa ilikuwa ianze kutekelezwa siku ya jumamosi.
Mahakama imefikia uamuzi huo mara baada ya watengezaji na watumiaji wa mifuko kupinga agizo hilo mahakamani huku wakisema kuwa kama itatekelezwa kwa agizo hilo basi watu 8000 watapoteza ajira zao.
Aidha, Watengenezaji wa mifuko hiyo ya plastiki pamoja na wafanyabiashara wa mifuko hiyo walienda mahakamani wakipinga ilani iliyotolewa na serikali inayopinga utengenezaji na uagizaji wa mifuko ya plastiki kutoka nje.
Hata hivyo, Wizara ya Mazingira inchini humo imesema kuwa mtu yeyote atayekutwa akitengeneza ama kufanya biashara ya mifuko ya plastiki atatumikia kifungo kisichopungua mwaka mmoja ama faini isiopungua dola 19, 000 za Marekani