Serikali imetoa siku saba kwa shirika la wakimbizi duniani UNHCR kuwarudisha wakimbizi wa Burundi ambao wanataka kurudi kwao kwa hiari ama sivyo serikali yenyewe itafanya zoezi hilo yenyewe.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alipokuwa katika ziara ya kikazi katika kambi ya nduta ambayo ni moja ya kambi zinazohifadhi wakimbizi wengi kutoka nchini Burundi.

Nchemba amesema kuwa maafisa wa shirika la wakimbizi duniani UNHCR ndio wanaochelewesha zoezi zima la kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa Burundi wanaotaka kurejea nchini kwao kwa hiari.

Aidha, zaidi ya wakimbizi elfu 8 kati ya laki moja ishirini na sita elfu katika kambi ya Nduta, ambayo Waziri Nchemba ameitembelea wamejiandikisha kurudi nchini mwao kwa hiari ili kuweza kuendelea na maisha.

Hata hivyo, Nchemba ameonya kuwa ikiwa UNHCR haitaanza zoezi la kuwarudisha wakimbizi hao, basi serikali italazimika kufanya yenyewe na kwamba itaomba magari kutoka jeshini ili kutekeleza zoezi hilo

Mahakama nchini Kenya yaitunishia misuli Serikali
Magazeti ya Tanzania leo Agosti 26, 2017