Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ziara ya kushtukiza katika wilaya ya Kigamboni na kuzungumza na wananchi katika eneo la feri pamoja na vijibweni katika daraja la Mwalimu Nyerere

Amesema kuwa anawashukuru wananchi waliojitokeza kumlaki kutoka kivukoni hadi anaondoka katika wilaya hiyo ambayo alifanya ziara hiyo ya ghafla kwa malengo ya kujionea vitu mbalimbali.

Aidha, katika hatua nyingine, Rais Magufuli amezungumza na wanachama wa CCM waliopo katika kambi ya mafunzo ya vijana iliyoandaliwa na umoja wa vijana wa vyuo na vyuo Vikuu (CCM) katika ukumbi wa chuo cha kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini Dar es salaam. TAZAMA PICHA ZAIDI

Ziara ya Majaliwa nchini Cuba kuinufaisha Tanzania
Serikali yawafunda mawaziri wa Afya wa Afrika