Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuagiza Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuwakamata Askari wote waliobainika kushirikiana na wauzaji wa dawa za kulevya na wale wanaobambikizia Wananchi kesi kukamatwa ndani ya masaa matano.

Makonda ametoa agizo hilo baada ya kubaini uwepo wa Askari wanaowalinda wafanyabiashara wa dawa za kulevya. Amesema wapo Askari wa uwanja wa ndege wanaoshirikiana na raia wa China kusafirisha Kobe na Wanyamapori, pia Askari wanawabambikia kesi wananchi ikiwemo wale wanaowakamata watu kwenye sehemu za mapumziko.

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 26, 2017
Video: Makonda apokea Pikipiki 10 za Askari wa usalama barabarani