Mahakama ya Kimataifa ya makosa ya Jinai, ICC, imeamuru kulipwa fidia ya dola milioni 10.kwa watoto walioingizwa katika kikundi cha Thomas Lubanga na kutumikishwa kama wanajeshi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
Thomas Lubanga ambaye aliitikisa DRC kivita alihukumiwa kifungo cha miaka 14 kwa makosa ya kuwateka watoto wadogo ambao wengine walikuwa chini ya miaka 11.
Aidha, Watoto hao walilazimishwa kupigana katika eneo la Ituri lililopo Mashariki mwa DRC ambapo ndipo ilipokuwa ngome kuu yaa kundi hilo.
Mawakili watetezi wa watoto hao walijenga hoja na kufanya utafiti juu ya maisha ya watoto hao na kubaini kuwa wanaweza kulipwa fedha nyingi ambazo zitawasaidia katika maisha yao.
-
Mrithi wa Mugabe aanza kusaka ‘huruma’ ya Magharibi
-
Hijab yazua gumzo, msichana azuiwa kwenye ‘graduation yake’
-
Marekani yaivuta Korea Kaskazini mezani
Hata hivyo, baada ya watoto hao kukombolewa kutoka katika mikono ya watekaji, wengi wao wakiwepo wasichana wamekataliwa kuungana na jamii zao.