Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru Serikali kuhakikisha Miguna Miguna anafika mahakamani Maei 18 mwaka huu kusikiliza kesi inayomkali.
Jaji wa mahakama hiyo, Chacha Mwita amesema kuwa Miguna anapaswa kuruhusiwa kuingia nchini na anatakiwa kutoa utetezi wake pamoja na vielelezo mwenyewe.
“Ninategeamea Miguna kuwa mahakamani hapa kusikiliza kesi inayomkabili ambayo itaendeshwa siku hiyo kwa kusikiliza ushahidi wake kutoka mdomoni kwakye yeye mwenyewe,” alisema Jaji.
Machi 26, Miguna alishikiliwa katika uwanja wa ndege jijini Nairobi akijaribu kuingia nchini humo kutoka Canada alikopelekwa kwa nguvu hapo awali. Baada ya mzozo wa siku moja, Miguna alisafirishwa tena bila hiari yake kupitia Dubai hadi nchini Canada.
Serikali ya nchi hiyo ilikana kutofuata taratibu na sheria kwa kumzuia Miguna kuingia nchini humo bali ilidai mwanasheria huyo alishindwa kukamilisha taratibu za kuwasili nchini humo kupitia uwanja wa ndege.
Miguna anadaiwa kutokuwa raia wa Kenya baada ya kuukana uraia wake na kubaki na uraia wa Canada. Mwanasheria huyo amepinga madai hayo ya Serikali ya Kenya, akisema ingawa aliwahi kuchukua uraia wa Canada hajawahi kuukana uraia wa Kenya. Ameitaka Serikali hiyo kutoa nyaraka zinazoonesha aliukana uraia wa Kenya.
The ministry had denied that Miguna was being held illegally this week and said he had failed to follow arrival procedures when he landed in Kenya.