Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa ushahidi wa vipisi vya bangi uliowasilishwa na upande wa mashtaka dhidi ya mshitakiwa ambaye ni muigizaji wa filamu, Wema Sepetu kwenye kesi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi inayomkabili.
Hakimu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba amesema kuwa ushahidi huo hauwezi kupokelewa kwa sababu una kasoro na kwamba shahidi hakuvifafanua alipouwasilisha mahakamani hapo.
Awali, wakili Tundu Lissu ambaye anamtetea Wema akisadiana na Peter Kibatala aliiomba mahakama hiyo kutopokea bahasha yenye vipisi vya bangi na vitu vingine iliyowasilishwa kama ushahidi na upande wa Jamhuri kwa madai kuwa kuna baadhi ya vitu ambavyo vimejumuishwa ambavyo havikutajwa mwanzoni.
- Lwandamina ampoteza baba yake mzazi,kuondoka leo kwenda Zambia
- Jux akumbukia mapenzi yake na Vanessa, asema haya kuikaribisha siku yake ya kuzaliwa
Upande wa mashtaka ulieleza kuwa bahasha hiyo ina vitu ambavyo vilikutwa katika nyumba ya Wema Sepetu wakati walipoenda kufanya ukaguzi. Pamoja na vitu vingine, walidai kuwa walikuta vipisi vya mabaki ya bangi ambavyo hata hivyo Lissu aliitaka mahakama kutovikubali akidai sio bangi.