Miaka 150 kutoka sasa, hakuna hata mmoja wetu anayesoma chapisho hili leo ambaye atakuwa hai na asilimia 70 hadi 100 ya kila kitu tunachopigania hivi sasa kitasahaulika kabisa.
Ikiwa tutarudi nyuma kwenye kumbukumbu za kiduania hadi miaka 150 nyuma itakuwa mwaka 1872, na hakuna hata mmoja wa magwiji wale waliobeba ulimwengu juu ya vichwa vyao walio hai hii leo.
Na ni wazi kuwa sisi sote tunasoma andiko hili tutapata ugumu wa kupiga picha uso wa mtu yeyote wa enzi hiyo, hivyo yatupasa kutulia kwa muda ili tufikirie jinsi baadhi yao walivyosaliti jamaa zao na kuwauza kama watumwa kwa vipande vya sarafu au nguo.
Adolf Hitler.
Wengine waliwaua washiriki wa familia kwa ajili tu ya kipande cha ardhi au mizizi ya viazi vikuu au Ng’ombe au kwa chumvi kidogo, shanga au vioo.
Bidhaa hizi za Viazi vikuu, Ng’ombe, kioo, au chumvi waliyokuwa wakitumia kujisifia iko wapi? inaweza kuwa hali ya kuchekesha kwetu kwasasa, lakini ndivyo sisi wanadamu tulivyo wajinga wakati mwingine, haswa linapokuja suala la pesa, nguvu au kujaribu kuwa muhimu!
Hata unapodai umri wako ni mdogo basi mtandao utahifadhi kumbukumbu yako, chukulia mfano wa Michael Jackson yeye alikufa mwaka 2009, sasa ni miaka 13 tu iliyopita.
Idd Amini Dada
Fikiria ushawishi ambao Michael Jackson alikuwa nao ulimwenguni kote alipokuwa hai na je ni vijana wangapi wa siku hizi wanaomkumbuka kwa hofu, yaani ikiwa hata wanamfahamu?
Katika miaka 150 ijayo, jina lake, likitajwa, halitapiga kengele kwa watu wengi hivyo yatupasa tuyachukulie maisha kwa urahisi, maana hakuna mtu atakayetoka katika ulimwengu huu akiwa hai.
Nchi unayopigania na uko tayari kuua, kumbuka kwamba mtu wa zamani aliiacha ardhi hiyo, mtu huyo amekufa, ameoza, na amesahauliwa na ndivyo itakavyokuwa pia katika hatima yako.
Biashara ya Utumwa.
Katika miaka 150 ijayo, hakuna gari au simu tunayotumia leo kujisifu ambayo itakuwa muhimu hivyo bado nasisitiza sana kuyachukulia maisha kwa urahisi na ongeza upendo kwa watu na upendo hhuo ukuongoze.
Muhimu ni tuwe na furaha ya kweli kwa kila mmoja, hakuna ubaya, hakuna kusengenya, hakuna wivu, hakuna kulinganisha na tambua ya kwamba maisha sio mashindano.
Mwisho wa siku, sote tutasafiri kwenda upande mwingine. Fumbo kubwa tulilonalo ni je? nani atatangulia kuondoka, huku tukitafakari kuwa sote tutaenda huko siku moja.