Wadau wa soka nchini Tanzania hususan vyombo vya habari wamekumbushwa kuwa na hali ya utulivu na kustahamili maisha ya baadhi ya wachezaji, ambao wamejiwekea malengo ya kucheza soka katika klabu moja ama nyingine pasina kuhoji muda.

Ushauri huo kwa wadau wa soka nchini Tanzania umetolewa na @Cubic chomox, kufutia sakata la kiungo wa mabingwa wa soka Tanzania bara Simba SC, Said Hamis Ndemla, ambaye mkataba wake utafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Tayari kiungo huyo mwenye sifa ya kupiga mashuti makali yanayolenga lango la timu pinzani kila anapopata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Simba SC, ameanza kuhusishwa na taarifa za kuondoka Msimbazi, huku klabu kama Young African, Polisi Tanzania na Namungo zikitajwa kuwa katika hatua ya kuiwania saini yake, japo haijathibitika.

Mdau wa soka @Cubic chomox, ameandika makala aliyoipa kichwa cha habari: MAISHA YA NDEMLA NI BORA KULIKO MATAMANIO YENU.

Naomba niwatakie mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ndugu zangu waislam walio katika toba, baada ya hapo niongee kidogo na watanzania “wenye nia nzuri” na Said Ndemla kuliko yeye alivyo na nia nzuri na maisha yake.

Naifaham kiu ya watanzania kumuona Ndemla akiwa katika kikosi cha kwanza cha Simba SC na Taifa Stars au hata Kagera Sugar kwa kuwa tunaamini uwezo huo anao, sikatai katika hilo na nakubaliana nanyi kwa asilimia nyingi kwa mkiwazacho, lakini je mmeifikiria kesho ya huyu mchezaji tunaetamani aondoke Simba kwenda kukuza kipaji katika umri huo?? Au mnazifikiria furaha zenu mtakapomuona anatawala dimba pale taifa mkasahau mpira ukiisha nyie mnarudi na furaha kwenu yeye aanze kuwaza anamalizaje madeni ya mtaani na wana mwezi wa nne huko alipo hawajalipwa?? Mnalifikiria hili kweli au ndo atajijua mwenyewe??

MPIRA NI AJIRA:

Hili ni jambo linalopigiwa kelele na wadau wa soka kila kukicha kuzisihi klabu zetu kuboresha maisha ya wachezaji wao maana sasa hivi ni ajira nzuri kwa vijana, mpaka kufikia hapa ni vilabu vitatu tu ambavo angalau kwa asilimia 60-70 wanawalipa wachezaji wao vizuri ambavyo ni Simba, Yanga na Azam FC hivyo mnapomshauri Ndemla kwenda sehemu nyingine kutafuta maisha nje ya Simba kwa lengo la kulinda kipaji chake je, mshajiuliza akitoka hapa anakwenda wapi?

Azam FC wanamhitaji jibu hapana, Je Yanga wanamhitaji tetesi zinasema ndio wanamhitaji, je wapo tayari kumpa alichokua anapata Simba? Jibu ninaamini hapana sasa aende wapi Kagera Sugar, Namungo au Polisi Tanzania FC?

Atapata namba huko lakini vipi atalipwa shilingi ngapi mnajua ana familia ya ukubwa gani inayomtegemea au mnataka kesho yake iwe ya majuto muanze kumcheka? tumezoea sana kuendeshwa na hisia za nje kuliko uhalisia na tumewapoteza watu wengi sana anachofanya Ndemla sio kigeni duniani maana yupo klabu anayoipenda halafu inalipa vizuri sasa anataka nini maishani? muda mwingine mpira ni bahati tu ndo utatoboa.

VAA VIATU VYAKE:

Wengi wanamshauri Ndemla aondoke simba kuokoa kipaji chake wakiwa na maana asiangalie maisha huku wao wakiwa wanafanyia kazi sehemu ambazo sio stahiki kwao na wengi wanaomshauri Ndemla kuondoka simba kuokoa kipaji bila kujali maisha yake baada ya kustaafu soka, wao wamekalia viti maofisini kwenye kazi ambazo hawana taaluma nazo au kipaji nazo wakiwazibia nafasi watu wenye weledi na hizo nafasi ila kwa sababu tu wanalipwa vizuri, wanaangalia nafasi zao na familia zao wanajenga kesho yao huwezi kuwalaumu hata, shirikisho linaendeshwa na madokta wa mifugo, radio zina watangazaji wachekeshaji vijana wenye vipaji na elimu wapo mtaani, mabondia wanachezasha mpira, klub zetu zinaongozwa na walanguzi.

Kabla hamjamjadili sana Ndemla tuyajadili maisha ya mtanzania je ni nani yupo tayari kuacha mshahara mzuri kwenda kulipwa kidogo ili tu amfurahishe baba mkwe wake au jirani yake? Yupo binadamu huyo hapa kwetu? hebu tafakari hilo.

MISHAHARA:

Kwa taarifa nilizonazo (sio rasmi) mchezaji anaelipwa mshahara mdogo Simba ni Rashid Juma, analipwa Milioni 1.5 mpaka laki 8 inacheza hapo, Said Ndemla inasemekana analipwa Milion 5-3 , ninazifahamu timu zetu za Tanzania ukitoa hao wakubwa 3 waliobaki sina hakika kama kuna mtu analipwa zaidi ya Milioni 2 atakaezidi sana anapokea Mil 1.5 sawa na Rashid wengine wote wanacheza laki 8 mpaka 5.

Turudi katika point ya msingi ingekua wewe ndio Ndemla ungeacha huo mshahara wa Simba uende kucheza sehemu utakayopunguza mshahara karibu mara 3 bado hautolipwa kwa wakati? Tuyafikirie maisha ya wachezaji wetu kabla ya kuwaandama, pia kumbuka ndemla kajijengea heshima na upendo kwa mashabiki wa Simba na viongozi wake.

Sehemu anayoweza kulipwa mshahara mkubwa kidogo na akapata namba ni Yanga, sehemu ambayo haitokua rafiki kwake maana anapoteza heshima kwa kipande cha fedha ambacho anakipata huku huku Simba SC pekee ambayo nitamshauri Ndemla aende kama watamhitaji kwa hapa Tanzania ni Azam FC tu bila kupepesa macho, hatapunguza mshahahara mkubwa pia atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Kama Azam FC hawamhitaji acheni Ndemla atengeneze maisha yake ya kesho hamtokuwepo akianza kupigika zaidi mtamcheka, wako wapi waliowasikiliza washauri wa mitandao na wako wapi hao wachezaji wa zamani waliokua wanajali uwezo wao walifika wapi.

Imeandaliwa na mdau wa soka: @Cubic chomox

CORONA: Fabregas atoa sadaka mshahara wake
Tanzia: Mkuu wa uhamiaji Kagera afariki Dunia