Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Jukwaa la Taasisi ya Wakurugenzi na wamiliki wa makampuni binafsi nchini (CEOrt) kushirikiana na serikali pamoja taasisi nyingine ili kubaini maeneo yenye uhitaji wa viongozi wakuu wazawa na kutoa mafunzo yenye tija.

Aidha, ameitaka Bodi ya Wakurugenzi wa Jukwaa hilo kuandaa mipango ya mafunzo yenye lengo la kutambua na kujenga uwezo kwa Watanzania katika sekta za kipaumbele hususan sekta ya madini, mafuta na gesi, ujenzi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Majaliwa ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam katika mahafali ya wahitimu wa Programu ya Uanagenzi kwa Maofisa Watendaji Wakuu (CEO Apprenticeship Program).

Jumla ya washiriki 16 wamehitimu mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Chuo cha Strathmore Business School (SBS) cha nchini Kenya, yameandaliwa na CEOrt kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira.

 

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Februari 2, 2021
Jeshi la Myanmar lafanya mapinduzi