Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, alitembelea banda la NSSF na kupata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele kuhusu ushiriki wa Mfuko katika Maonesho ya Wiki ya Vijana yanayoendelea Wilayani Bukoba Mkoani Kagera, ambapo Mfuko unatumia maonesho hayo kutoa elimu ya hifadhi ya jamii, kutambua na kuandikisha waajiri na wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kutatua kero za wanachama na kueleza fursa mbalimbali za Uwekezaji.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika banda la NSSF, walipatiwa elimu ya hifadhi ya jamii kuhusu umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba. Utoaji wa elimu ya hifadhi ya jamii uliongozwa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Kagera, Siraji Kisaki akisaidiana na baadhi ya wafanyakazi wa NSSF. NSSF ilishiriki Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kuandikisha wanachama, kusikiliza na kutatua kero pamoja na kueleza fursa mbalimbali zikiwemo za uwekezaji.Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya, alitembelea banda la NSSF wakati wa Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofikia kilele tarehe 14 Oktoba, 2022 Mkoani Kagera. Alipokuwa katika banda la NSSF alielezwa kuwa Mfuko ulishiriki Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi pamoja na kuandikisha wanachama, ambapo alipongeza kazi kubwa na mzuri inayofanywa na NSSF hasa katika kutoa elimu ya hifadhi ya jamii ambapo pia alifurahishwa na miradi ya nyumba inayotekelezwa na NSSF na kuwataka Watanzania kuchangamkia fursa ya kununua nyumba hizo kwani ni mzuri na za kisasa.
Baadhi ya wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa miaka tofauti wakiongozwa na Mwashibanda Shibanda, walitembelea banda la NSSF wakati wa Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofanyika Wilayani Bukoba Mkoani Kagera, ambapo Meneja wa NSSF Mkoa wa Kagera, Siraji Kisaka aliwaeleza ushiriki wa Mfuko katika maonesho hayo kuwa ni kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kuandikisha wanachama pamoja na kutatua kero. Aidha, Siraji aliwakabidhi zawadi za t-shirt.