Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezitaka serikali za vijiji na ngazi nyingine mkoani Pwani kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo yakiwemo ya viwanda ili kulinda mali na usalama wa wawekezaji na watanzania kiujumla.
Amesema kuwa haijajulikana hadi sasa nia na dhamira ya watu wasiojulikana wanaojihusisha kupoteza maisha ya watu na ni hatari endapo watajiingiza katika maeneo ya uwekezaji kwani hakuna mwenye uhakika wa azma yao.
Aidha Majaliwa ,ametoa wiki mbili kwa Waziri wa maji kutathmini matokeo ya mwenendo wa mradi wa maji wa WAMI ,ili kutoa utaratibu na kama sheria inaruhusu kuvunja mkataba ikiwa mkandarasi ameshafikia kiwango cha asimilia 50 ya utekelezaji.
“Hatuna uhakika kwa watu hawa wanaofanya vitendo vya ovyo, watanzania waungane na serikali,kupambana ili wasije kuingia kwa wawekezaji na kupoteza ndoto za serikali za kupata wawekezaji “amesema Majaliwa.
-
Gazeti la Mwanahalisi lafungiwa kwa uchochezi
-
Bombardier yapata hitilafu Jijini Mwanza
-
Kichanga chaokotwa na ujumbe mzito
Hata hivyo, katika hatua nyingine, Majaliwa ametoa wiki mbili kwa waziri wa maji na umwagiliaji kuweza kushughulikia mara moja tatizo hilo ambalo limekuwa kero kwa wananchi.