Msemaji wa Polisi Afrika Kusini katika mji wa East London, Nkosikho Mzuku ametangaza kuwa siku ya jumamosi mtoto wa kiume ameokotwa katika eneo lake huku akiwa amevirigwa t-shirt na kuachwa na ujumbe mzito kwa yeyote atakaye muokota.

Mtoto huyo mwenye umri wa siku tano ameokotwa na wapita njia katika mji huo Afrika Kusini akiwa kwenye mfuko wa takataka.

Ambapo msemaji amesema kuwa mtoto huyo alionwa na watoto waliokuwa wakipita kwenda kwa mwalimu wao na kukuta mfuko wa takatka uliovirigwa.

Kwenye mfuko huo walikuta kikaratasi chenye ujumbe ambao unaaminika kuwekwa na mama yake, akiomba kwa yeyote atakayemuokota mtoto huyo ampeleke sehemu salama.

“Tafadhali mchukue mtoto huyu na mpeleke kituo cha polisi, baba yake anataka kumuuza, nimekimbia naye lakini najua atatutafuta, ni bora nife mimi kuliko mtoto kwa sababu hana hatia, nimejifungua mtoto huyu Septemba 14, 2017, ahsanteni na Mungu akubariki”, ulisomeka ujumbe huo ambao ulikutwa kwa mtoto huyo.

Jeshi la polisi nchini Afrika Kusini limesema linaendelea kumtafuta mama wa mtoto huyo na kumtia mikononi mwa sheria.

 

Kikwete asikitishwa na uzushi unaozagaa mitandaoni
Video: Wafuasi wa Jubilee waandamana Kenya