Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa uchungu anaoupata baada ya kuunguliwa na nyumba yake umemfanya kuwafikilia wananchi wanaobomolewa nyumba zao bila fidia.

Ameyasema hayo kupitia ukurasa wake Facebook mara baada ya kuitazama nyumba yake ya kwanza iliyoteketea kwa moto mwishoni mwa wiki iliyopita huko Mwandiga mkoani Kigoma.

“Sikudhani kabisa kuwa naweza kuumizwa na kupata uchungu kwa tukio kama hili na ninajiuliza huu uchungu ni wa nini? Kumbe ni uchungu wa nyumba ya kwanza. Nawafikiria wananchi wenzangu wanaobomolewa nyumba zao bila fidia, na wengi ni nyumba zao za kwanza na pekee. Uchungu wao nausikia. Hasira zao nazihisi,”amesema  Zitto

Amesema kuwa ameridhika kwa kile  kilichotokea kwenye nyumba yake kuungua moto kwakuwa ni ajali ya kawaida na wala watu wasichukulie kwa muktadha wa matukio yanayoendelea nchini kwa sasa.

Hata hivyo, Nyumba ya Zitto Kabwe iliyoungua hivi karibuni huko Mwandiga Mkoani Kigoma inadaiwa kuwa ndiyo nyumba yake ya kwanza baada ya kupata  ridhaa ya kuwa mbunge.

 

Bombardier yapata hitilafu Jijini Mwanza
Sentensi 4 tata zilizomkera Zari wa Diamond