Kupitia kipindi cha Leo tena Clouds FM, Diamond Platinumz amefunguka na kuweka wazi mambo makubwa ambayo amemfanyia Hamisa Mobeto tangu kipindi ana ujauzito wake mpaka sasa ambapo amejifungua salama mtoto Abdul au Diylan.

Pindi akihojiwa Diamond amezungumza mambo makubwa ambayo mpenzi wake Zarina hakuyajua yalikuwa ‘exclusive’ kama ilivyo kwa watazamaji na wasikilizaji wengine wa kipindi hiko ambacho Diamond amefungua moyo na kuweka hadharani kila kitu kiasi cha kumkasirisha mpenzi wake Zari.

Inasemekana kuwa sentensi tano alizoongea Diamond na kumtoa Zarina povu ni;

1. Baada ya Hamisa kuwa na kibendi Diamond alimnunulia gari aina ya Rav 4 ili imsaidie kwenda cliniki”

2. Pindi Hamisa akiwa na ujauzito nimekuwa nikimpa elfu sabini kwa siku ambayo ni sawa na laki tano kwa mwezi na baada ya kujifungua nilimpa Hamissa Milioni 7, kwa ajili ya matumizi na kumnunulia mtoto kila kitu ili akue katika mazingira mazuri”.

3.  Na kipindi chote ambapo taarifa zimekuwa zikisambaa kuhusu ujauzito Zari alikuwa anajua kila kitu”’

4. Nilimwambia kabisa fulani ana ujauzito wangu, Zari ni mtu mzima alinielewa tukasameheana , Zari hana noma kabisa na huyu mtoto”

5. Hapo ndipo Povu lilipomtoka Zari na kumwambia mpenzi wake achunge sana maneno yake, na aache uongo apambane na matatizo yake, Zari akamalizia kwa kusema.

”Ukimya wangu haimaanishi mi mjinga”  amesema Zari

Ni kweli Zari ana pesa za kutosha na Diamond kumpa Pesa Hamisa sio kitu kikubwa sana ili kitendo cha Diamond kumficha Zari mambo yanavyoendelea na kujinadi kwenye vyombo vya habari kuwa mke wake anajua kila kitu na ameshamsamehe, Zari ameita kitendo hiko ni kitendo cha uongo na uchonganishi.

Aidha Diamond amefanya jambo jema kumkubali mtoto wake, pia amewaomba radhi mashabiki wake na familia yake kwa kile ambacho kimetokea kutokana na ujinga wake.

 

Zitto: Nimeumia sana nyumba yangu kuteketea kwa moto
Gazeti la Mwanahalisi lafungiwa kwa uchochezi