Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameagiza kufanya uchunguzi katika Kampuni ya TANCOAL ili kujiridhisha kama mapato yanayoingizwa na Kampuni hiyo ni halali.
Ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya mgodi huo baada ya kufanya ziara ya kuutembelea mgodi huo kujionea shughuli za uzalishaji zinazofanyika.
Majaliwa amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ya Serikali (CAG) ili apitie mahesabu ya kampuni hiyo tangu mwaka 2011 walipoanza uzalishaji.
“Desemba 2013 mliuza tani 39,000 kwa wamiliki wa viwanda vya nguo, pia mliuza tani 2,000 kwa Kampuni ya Saruji ya Zambia, Novemba 2013 mliingia makubaliano ya kuuza tani 165,000 kwa kampuni ya saruji ya Tanzania na ziliuzwa. Mbona ‘financial statement’ zenu zinasema mwaka huo nao mlipata hasara?” “Mnasema gawio  hutolewa baada ya mtu kutangaza faida. Mbona mlivuka lengo lakini mkatangaza kuwa kampuni imepata hasara katika mwaka huo wa fedha?” amesema Majaliwa.
Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa kampuni ya TANCOAL, uongeze uzalishaji ili uweze kukidhi mahitaji ya ndani, kwani makampuni mengi yamebaini gharama kubwa iliyopo kwenye matumizi ya mafuta ya dizeli na sasa yanahitaji makaa ya mawe kwa uzalishaji.

Kesi ya uhujumu uchumi yakwama
Gambo awabebesha zigo Wakuu wa Wilaya Arusha