Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaja sababu ya baadhi ya mabalozi kurejeshwa nchini muda mchache baadaya uteuzi kuwa ni kutokana na kushindwa kufanya chochote katika kutangaza utalii wa nchi.
Amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa dini nchini ambapo amesema kuwa serikali imetangaza mpango mahususi kwa ajili ya utalii wa nchi kwa mabalozi wote wa Tanzania ambapo imekuwa ni moja ya jukumu la mabalozi hao.
“Changamoto tuliyonayo ni baadhi ya mataifa kutangaza vitu vyetu kuwa ni mali yao, lakini tumeshaandaa mpango kupitia mabalozi wote wa Tanzania walioko kwenye nchi mbalimbali, moja kati ya jukumu lao ni kutangaza utalii wa nchi” amesema Waziri mkuu.
“Hatuwezi kukutambua kuwa wewe ni balozi wetu ukatutangaze alafu unakaa miezi mitatu au sita huna jambo la kufanya si bora urudi, wote wanajua na tunasimamia, kwahiyo mkisikia mtu ameenda na kurudi msishangae,” amesema Majaliwa.
Aidha, waziri mkuu amewakumbusha viongozi wanaopata fursa zakuzungumza mbele za watu kuacha maneno yenye kuondoa utu, dharau na hata kuvunjiana heshima hususa ni kuelekea kipindi cha kampeni.
Uchaguzi Mkuu nchi Tanzania kufanyika Jumatano Oktoba 28 badala ya 25,ambapo Waziri Mkuu Majaliwa amefafanua kuwa waliamua kufanya hivyo kutokana na kutambua mchango wa dini na kuondoa kero iliyokuwa ikijitokeza dakika za mwisho.