Kampuni ya Dawa ya Ujerumani, BionTech imeanza kufanya majaribio ya chanjo ya malaria ili kujua usalama na ufanisi wa chanjo hiyo inayoitwa BNT165b1, ya awamu ya kwanza.
BionTechWatu imesema, watakaofanyiwa majarabio hayo wataangaliwa katika viwango vitatu tofauti vya dozi ambapo asilimia 95 ya watu wanaougua malaria na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vilitokea barani Afrika.
Mwanzilishi mwenza wa BionTech, Ozlem Tureci amesema kuanzishwa kwa majaribio hayo ni hatua muhimu katika juhudi zao za kusaidia kukabiliana na magonjwa yenye uhitaji mkubwa wa matibabu.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani, WHO, takribani watu 619,000 walikufa duniani kwa kuugua malaria mwaka 2021, ikiwa ni idadi pungufu ya watu 625,000 mwaka uliotangulia.