Jeshi la Polisi, Kupitia Kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na Polisi Mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa madawa ya kulevya Pamoja na vifaa mbalimbali.

Mkuu wa Polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya nchini, Kamishina msaidizi wa Polisi, ACP Amon Kakwale.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo Desemba 23, 2022 na Mkuu wa Polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya nchini, Kamishina msaidizi wa Polisi, ACP Amon Kakwale amesema kuanzia mwezi Julai hadi Novemba, 2022, jumla ya kesi 369 zilifikishwa mahakani na kutolewa uamuzi.

Boti mbili zilizokamatwa na kutaifishwa.

Amesema, jumla watuhumiwa 377 walitiwa hatiani kwa makosa ya kujihusisha na madawa ya kulevya na kwamba watuhumiwa 170 walifungwa vifungo mbalimbali kwa makosa hayo, huku vyombo vya moto vilivyo kamatwa na kutaifishwa Mahakama kuwa Mali za Serikali vikiwa ni Magari 8, Pikipiki 9, Boti 2 na Nyumba moja.

Miongoni mwa pikipiki ambazo zilizopo kituno zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali.

Aidha, kakwale amesema Jeshi hilo halitosita kumchukulia hatua mtu yeyote atakaye kamatwa akijihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na linawaomba wananchi kutoa taarifa za watu wachache wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ili hatua zichukuliwe dhidi yao.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 24, 2022
Aliyejaribu kuuwa kwa kisu jela miaka 14