Ili kuhakikisha huduma za Afya zinaendelea kuimarika ngazi ya Jamii, nguvu za pamoja zinahitajika ambapo Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imekuwa mstari wa mbele kwa kuweka mikakati mbalimbali ya uboreshaji wa huduma.

Afisa Program huduma za afya ngazi ya jamii, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma,Idara ya Kinga,Wizara ya Afya, Orsolina Tolage ameyasema hayo Mkoani Morogoro, katika kikao cha pamoja kilichoandaliwa na asasi ya kiraia ya SIKIKA kupitia mfuko wa dunia, Global Fund.

Afisa Program huduma za afya ngazi ya jamii, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma,Idara ya Kinga,Wizara ya Afya, Orsolina Tolage (aliyesimama), akiongea wakati wa kikao hicho.

Amesema, ni muhimu kuimarisha huduma za afya ngazi ya jamii kwani ndio kiunganishi kutoka kwenye jamii hadi katika vituo vya kutolea huduma za afya huku kikao hicho kikitajwa kuleta manufaa katika utekelezaji wa program ya afya ngazi ya jamii ikiwemo mikakati ya usafi wa mazingira.

Kikao hicho, kililenga kujadili mafanikio, changamoto na kupeana uzoefu wa utekelezaji huduma za afya ngazi ya jamii katika afua za UKIMWI, Kifua kikuu (TB) na Malaria.

Mifugo 2035 yakamatwa Hifadhini, sita washikiliwa na Polisi
Wazazi wahimizwa kutoa Elimu ya Afya kwa Vijana