Mamia ya Wanawake wamekusanyika nje ya Chuo Kikuu cha Kabul nchini Afghanistan kupinga uamuzi wa Serikali ya kuwazuia kujiunga na elimu ya chuo kikuu.

Maandamano hayo, yanatajwa kuwa makubwa kutokea hadharani katika mji huo tangu Taliban ilipotangaza uamuzi wake wa kufunga vyuo vikuu vya wanafunzi wa kike.

Sehemu ya waandamanaji Wanawake wa Taliban wanaopinga zuio la Serikali la kujiunga na vyuo vikuu. Picha ya Al Jazeera.

Kufuatia hatua hiyo, hali ya usalama imeimarishwa kwenye maeneo ya vyuo vikuu huku uamuzi huo wa Taliban ukikosolewa na jumuiya ya Kimataifa, nchi ya Saudi Arabia na Uturuki ambazo nazo ni Mataifa ya kiislamu.

Desemba 22, 2022 Serikali ya Uturuki, iliwataka watawala wa Serikali ya Taliban nchini Afghanistan kutengua uamuzi wao wa kuwazuia wanawake kujiunga na vyuo vikuu, ikisema kitendo hicho sio cha kiislamu wala ubinadamu.

Wazazi wahimizwa kutoa Elimu ya Afya kwa Vijana
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 23, 2022