Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa ni mchango mkubwa katika kufanikisha mradi wa ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), kutokana na kujipanga na kuulinda tangu awali hadi kukamilika kwake.

Makamba ameyasema hayo hii leo Desemba 22, 2022 wakati akiongea katika tukio la ujazaji maji Bwawa la Mwalimu Nyerere ambao utashuhudiwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa, Vyama, Serikali na Wananchi, huku ukitarajiwa kusaidia uchumi wa nchi.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba.

Amesema, “Kwa namna ya kipekee nivishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa mchangao wao mkubwa, walijipanga na kuhakikisha wanalinda miundombinu ya mradi tangu mwanzo na kuhakikisha kila kityu kinakuwa salama toka kuanza kwake mpaka hii leo.

Aidha, Waziri Makamba amesema Rais Samia pia alielekeza kuwa kutokana na umuhimu wa hatua hiyo, Watanzania wanatakiwa kuzitambau jitihada za Marais waliopita katika kuiweka hai ndoto ya mradi huu, akiwemo muasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere.

Bodi ya Wakurugenzi TAWA yafanya ziara ya kikazi Pori la akiba Kirejeshi
Agram Grant atua rasmi Chipolopolo