Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Ramadhan Mgunda, amesema mchezo wa kesho Alhamis (Mei 09) dhidi ya Azam FC utakuwa ni kama Fainali, ili kufanikisha mpango wao wa kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu ujao.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mgunda amesema mchezo huo utakuwa mgumu, lakini amekiandaa kikosi chake kwenda kupmbana na kuhakikisha kinaibuka na ushindi.

“Tunakutana na Azam FC, mchezo utakuwa mgumu sana na tunaweza kusema ni fainali kwa sababu ndio unaotoa taswira ya kushika nafasi ya pili kwa sababu tunahitaji kumaliza kwenye nafasi hiyo,” amesema Mgunda na kuongeza;

“Si rahisi, lakini naamini nitaisaidia Simba SC irudi kwenye ushindani, ninaimani wachezaji watairudisha timu sehemu nzuri. Vijana waliopo wote wamepevuka na wanaelewa namna ya kufanya ili kuiweka timu katika ushindani, hivyo cha muhimu ni kuwajenga kisaikolojia na kuwarudisha kwenye morali na kila kitu kitakuwa sawa,” amesema

Young Africans ipo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na alama 65, ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 57 huku Simba SC ikishika nafasi ya tatu kwa alama zake 53, lakini ikiwa na mchezo mmoja mkononi, hivyo kama ikishinda michezo yake yote sita iliyosalia itamaliza na alama 71.

Kwa upande wa Azam FC ambayo itakuwa mwenyeji wa Simba SC kesho Alhamis (Mei 09), ikishinda mechi zake zote tano zilizosalia itafikisha alama 72, jambo ambalo linaufanya mchezo wao huo kuwa muhimu kwa kila timu kuwania kupata matokeo chanya.

Makala: Hivi Waafrika ni nani aliyeturoga
Mwamba anarudi tena nyumbani