Ripoti ya Wataalam huru wa Umoja wa Mataifa (UN), inaeleza kuwa Jeshi la Rwanda lilihusika kwenye operesheni za kijeshi dhidi ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika maeneo yanayokumbwa na machafuko mashariki mwa DRC.

Wataalam hao, wamesema kuna ushahidi wa kutosha kwamba jeshi la Rwanda liliingilia kati moja kwa moja katika vita vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, dhidi ya waasi wa kundi la M23.

Kikosi cha walinda amani Goma, DRC. Picha ya DW.

Aidha, ripoti hiyo pia imeeleza kuwa, Jeshi hilo liliwaunga mkono waasi hao kwa kuwapa silaha, risasi na magwanda au sare za kivita na kwamba Rwanda iliwaimarisha wanamgambo wa M23 kwenye operesheni maalum, zilizolenga kukamata miji na maeneo ya kimkakati.

Hata hivyo, ripoti hiyo inaelekeza kuwa Wanajeshi wa Rwanda pia waliongoza mashambulizi ya pamoja na wanamgambo wa M23 dhidi ya maeneo ya wanajeshi wa Congo mwezi Mei huku msemaji wa Serikali mjini Kigali akikanusha madai kwamba Rwanda iliwaunga mkono waasi hao.

Czeslaw Michniewicz amaliza kazi Poland
Gabriel Jesus airudisha sokoni Arsenal