Wataalamu wa masuala ya kijasusi wa Umoja wa Mataifa, wamebaini operesheni zinazoshukiwa kuwa za waasi wa M23 kwenye maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC.
Kupitia nyaraka za ndani za Umoja huo, zimeonesha kuwa M23 wamedhibiti maeneo mengine, wakati ambapo walitakiwa kuondoka na kitendo cha kusema wameyaacha maeneo ya jimbo la Kivu Kaskazini na mji wa Kibumba hakina ukweli.
Aidha, ripoti hiyo imeleeza kuwa mapigano kadhaa yanayowahusisha M23 yameripotiwa wiki hii na kusababisha waasi hao kudhibiti maeneo zaidi, ikiwemo lile la Kitchanga na Nyamilima hali inayoleta wasiwasi kwa raia.
M23, walipaswa kuondoka pia kwenye mji wa kimkakati wa Rumangabo lakini siku ya Jumatano (Januari 4, 2023), Kikosi cha Jumuia ya Afrika Mashariki kiliahirisha hafla iliyopangwa ya makabidhiano, kikisema bado kinatathmini hali ya usalama.