Takriban watu 16 wamefariki na wengine 21 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuelekea Gulu kugonga Lori katika kituo cha biashara cha Adebe kilichopo Kamdini kando ya barabara kuu ya Kampala-Gulu kaskazini mwa Uganda.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi la Polisi eneo la Kyoga Kaskazini, Patrick Jimmy Okema amesema katika ajali hiyo watu 12 walifariki papo hapo huku wengine wanne wakifariki katika hospitali ya Atapara ambako walikuwa wamekimbizwa kwa ajili ya matibabu.

Hali ya Basi hilo mara baada ya ajali katika barabara kuu ya Kampala-Gulu iliyotokea usiku wa kuamkia leo Januari 6, 2023. Picha ya Daily Monitor.

Amesema, “Basi lenye namba za usajili UAT 259P, la kampuni ya Roblyn, lilikuwa likitoka Kampala kwenda Gulu na liligonga trela usiku wa Januari 6, 2023 kwenye barabara kuu ya Kampala-Gulu. Trela ​​hilo lilikuwa likipakiwa katika kituo cha biashara cha Adebe kilomita moja kutoka kituo cha ukaguzi cha Kamdini.”

Aidha, Okema ameongeza kuwa, waliofariki walipelekwa katika walipelekwa katika kituo cha afya cha Anyeke Health IV, kwa ajili ya uchunguzi wa maiti huku akikisema chanzo cha ajali hiyo ni maegesho yasiyo sahihi ya dereva wa Lori bila kuweka alama za tahadhari.

Msifiche Mbolea sambazeni kwa Mawakala: RC Mrindoko
Kilichotokea TFF kesi ya Fei Toto, Young Africans