Msemaji wa Serikali ya Gambia, amesema Serikali nchini humo imewashtaki raia wake wawili na Afisa mmoja wa Polisi kwa tuhuma za kufanya jaribio la mapinduzi ya Desemba 21, 2022.

Hatua hiyo imejiri baada ya mamlaka za usalama kuzima mapinduzi ya kijeshi na baadaye kueleza kwamba watu hao waliopanga njama hizo za kutaka kuwakamata maafisa wakuu wa serikali na kuwatumia kama mateka, ili kuzuia nchi za kigeni kuingilia kati kijeshi.

Mahakama kuu nchini Gambia. Picha ya Justice Defenders.

Watuhumiwa hao ni Mustapha Jabbi, Saikuba Jabbi na Inspekta wa Polisi, Fakebba Jawara ambao kwa pamoja walikamatwa Desemba 30 na kushtakiwa kwa uhaini na kula njama ya kutenda uhalifu huku takriban wanajeshi saba nao wakikamatwa kwa kuhusika na nkesi.

Hili linatokea wakati ambapo tayari Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Unified Democratic Party (UDP), Momadou Sabally, aliachiliwa huru wiki iliyopita, ikiwa ni siku chache baada ya kukamatwa kwake kwa kuonekana kwenye video inayopendekeza Rais, Adama Barrow aondolewa madarakani kabla ya uchaguzi ujao.

Ally Kamwe: Nilishangaa alichoniambia baba
Simba SC yasitisha Dili la Kwame Opuku